Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAKUKURU kuwafikisha mahakamani vigogo saba TPA uhujumu uchumi

Arrested Crime.jfif TAKUKURU kuwafikisha mahakamani vigogo saba TPA uhujumu uchumi

Fri, 12 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) itawafikisha mahakamani watumishi nane wakiwemo saba wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kwa makosa ya rushwa, uhujumu uchumi na wizi wa zaidi ya Sh.8 bilioni.

Katika taarifa iliyotolewa mapema leo na afisa uhusiano wa taasisi hiyo, Doreen Kapwani, imesema kuwa uchunguzi wao umebaini kuwa pamoja na kosa hilo la uhujumu uchumi, watuhumiwa hao pia waliunda genge la uhalifu pamoja na kuwasilisha nyaraka za uongo.

"Sambamba na kuwafikisha watuhumiwa hao nane mahakamani leo, uchunguzi huu wa Takukuru bado unaendelea kwa lengo la kubaini kiasi kingine cha fedha zilizohujumiwa ikiwa ni pamoja na kuwatafuta na kuchukua hatua za kisheria," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Katika hatua nyingine, taasisi hiyo pia inawatafuta mfanyabiashara Chrispin Iranque mfanyabiashara pamoja na Arnold Temba, ambaye ni wakili na mkurugenzi wa kampuni ya Ela ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano ya kuhusika kwenye uhujumu uchumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live