Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steve ahukumiwa jela maisha kwa kumbaka mtoto miaka 7

Steve Ahukumiwa Jela Maisha Kwa Kumbaka Mtoto Miaka 7 Steve ahukumiwa jela maisha kwa kumbaka mtoto miaka 7

Wed, 27 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha maisha jela Steve Ngusi Mwenye umri wa miaka 20 baada ya kumkuta na hatia ya kumbaka Mtoto mwenye umri wa miaka saba aliyekuwa akisoma darasa la kwanza.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa amesema Mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo bila ya kuacha shaka kuwa Steve ametenda kosa hilo na ametiwa hatiani.

Siku ya tukio July 05, 2023 Mtoto huyo akiwa anatoka Shuleni alifikia dukani Kwa Babu yake ndipo Babu huyo akamtuma Steve kumpeleka Mtoto huyo nyumbani na Steve akampitisha katika jumba bovu na kumbaka, ilipofika jioni Bibi wa Mtoto aligundua Mjukuu wake hayupo sawa na alipomuuliza akamwambia alichofanyiwa na Steve.

Kesi hiyo imesimamiwa na Mwendesha mashtaka wa Serikali Sauli Makoli na ilikuwa na Mashahidi watatu akiwemo Daktari aliyempima Mtoto siku ya tukio na kuthibitisha kuwa alikuwa na michubuko ya kuingiliwa sehemu za siri.

Steve alipopewa nafasi ya kujitetea ameiambia Mahakama kuwa apewe adhabu ya kufanya usafi Mahakamani hapo lakini pia akadai ana matatizo ya kisaikolojia lakini hata hivyo Mahakama imemuhukumu jela maisha pamoja na fidia ya Tsh. milioni tano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live