Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siyanga: Aliyefia Mwananyamala hakuwa na dawa za kulevya tumboni

32733 Dawapic Tanzania Web Photo

Fri, 21 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) imesema uchunguzi uliofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili umebaini kuwa mwili wa mfanyabiashara, Happy Mboya (38) aliyefariki dunia katika Hospitali ya Mwananyamala haukuwa na dawa za kulevya.

Happy alifariki dunia Jumapili Desemba 16, 2018 na mwili wake ulipangwa kusafirishwa jana kwenda Moshi kwa mazishi lakini polisi kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam waliuchukua kwa ajili kuupeleka Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Desemba 21, 2018 Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo, Rogers Siyanga amesema, “maofisa wetu wa DCEA walikuwepo wakati mwili wa marehemu Happy unafanyiwa upasuaji. Haujakutwa na dawa za kulevya kama ilivyodaiwa.”

Jana Siyanga alilieleza Mwananchi kuwa baada ya uchunguzi huo angetoa taarifa kamili juu ya tukio hilo.

Baba mdogo wa marehemu, Ally Bilali jana alilieleza Mwananchi kuwa baada ya kurejea nchini, Happy alifikia katika nyumba ya kulala wageni ambayo haikufahamika na mtu mwingine isipokuwa mume wake.

“Hata dada yake alikuwa hafahamu kuwa amesharudi kwa sababu alidai kuwa simu yake imeharibika na wasingeweza kuwasiliana kumbe ilikuwa kumficha. Alipata taarifa baada ya mdogo wake kuzidiwa na wahudumu kumpigia simu ndipo alienda kumchukua kumuwahisha hospitalini,” amesema.

Amesema baada ya kufika hospitalini na kupimwa, alionekana kuwa na njaa kali jambo ambalo lilimlazimu daktari kumuandikia dripu za maji ili kumsaidia, “Lakini hizo dripu hakuwekewa na hatukuambiwa sababu ya msingi hadi alipofariki.”

 

Mwili wa Happy unaagwa leo Muhimbili.

 

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.

 

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz