Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sitta atajwa kesi uhujumu kigogo wa reli

SAMWEL SITTA Sitta atajwa kesi uhujumu kigogo wa reli

Thu, 7 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

Mchunguzi Mkuu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Malimi Mifuko, amedai kuwa aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, alikuwa akiufahamu mchakato wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kisasa.

Sambamba na kuufahamu mchakato huo, amedai kuwa Sitta (sasa marehemu), alitoa maelekezo kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Benhardard Tito.

Mifuko ni shahidi wa saba katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Tito na wenzake wanaotuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Maghela Ndimbo, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Joseph Luambano, shahidi huyo alidai walipokea malalamiko na kwamba yanapokuwepo lazima uchunguzi ufanyike.

Alidai kuwa walikusanya nyaraka ili kujiridhisha kama zabuni ya ujenzi wa reli ya kisasa ipo na katika uchunguzi walibaini zabuni ipo na mchakato ulishaanza.

Hata hivyo, shahidi huyo alidai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za ununuzi na hicho ni kiashiria tosha cha kuwapo kwa tatizo kwenye mchakato mzima wa zabuni.

Alidai alikusanya nyaraka kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya ukaguzi ikiwemo RAHCO kwa Mkaguzi wa Fedha, Mkaguzi wa Ndani, Benki ya CRDB na miongoni mwa nyaraka hizo ilikuwa nakala za mkataba wa ujenzi wa reli.

Shahidi anadai hawakupata mkataba halisi katika maeneo yote waliyoelekezwa na mshtakiwa wa kwanza, Tito.Alidai nyaraka mojawapo ilikuwa ya CRDB ya kuomba kufungua akaunti ya malipo ya Dola za Marekani 500,000 kwa Kampuni ya Rothschild ya Afrika Kusini na kulikuwa na maombi mengine ya malipo ya Dola milioni 100 kwa Kampuni hiyo ya Rothschild.

Chanzo: ippmedia.com