Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sita wakamatwa kwa kuiba nguzo 234 za taa za barabarani

12503 WATUHUMIWA+PIC TanzaniaWeb

Fri, 17 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro.Watu sita wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro, kwa tuhuma za kuiba nguzo 234 za taa za barabarani.

Pia watu hao walikamatwa wakiwa na pombe aina ya gongo lita 240 na lita zaidi ya 300 za mafuta ya dizeli ya mitambo inayotumika kutengeneza reli ya mwendokasi.

Akitoa taarifa hizo leo Agosti 17, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa amesema watuhumiwa wote wamekamatwa na uchunguzi unaendelea.

Kamanda Mutafungwa amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi.

“Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz