Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sita mbaroni kwa tuhuma za wizi, mali ya wizi

28200 Pic+wezi TanzaniaWeb

Thu, 22 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Watu sita wanashikiliwa na polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za wizi na kukutwa na mali zinazoaminika kuwa za wizi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amewataja wanaoshikiliwa kwa tuhuma za wizi kuwa ni William Alex (24), Peter Deogratius (22), David Yusuph (18) na Godfrey Joseph (28), wote wakazi wa Jiji la Mwanza.

“Polisi walifanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa hao baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu kuwapo kwa kundi la watu wanaovunja nyumba nyakati za usiku na kupora mali,” amesema Shanna.

Pia, amesema Polisi walifanikiwa kuwakamata Rashid Ramadhan (32) na Ester Izack (55) wote wakazi wa Jiji la Mwanza kwa tuhuma kupokea na kukutwa na mali inayoaminika kuwa ya wizi.

Miongoni mwa vitu wanavyotuhumiwa kuiba na kukutwa nazo ni pikipiki mbili, injini moja ya pikipiki, majokofu manne, luninga mbili, meza ya kuwekea luninga moja, kompyuta mpakato moja, kompyuta moja, redio mbili aina ya sabufa na spika zake saba, king’amuzi na rimoti tatu, pasi za kunyoshea nguo mbili.

Vingine ni jiko la gesi la kupikia, sufuria 10 za kupikia, magodoro mawili na mashuka mawili, mitungi miwili ya gesi, mashine ya kupima msukumo wa damu, nguo aina mbalimbali zilizofungwa kwenye mafurushi mawili, chupa tupu za bia na bidhaa mbalimbali za dukani.



Chanzo: mwananchi.co.tz