Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sita kortini wizi mawe ya dhahabu

Hukumu Pc Data Sita kortini wizi mawe ya dhahabu

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu sita wakazi wa wilaya ya Geita, wamefikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo, wakikabiliwa na shtaka la wizi wa kilo 54.1 za mawe yanayosadikiwa kuwa na dhahabu.

Washtakiwa hao Musa Ramadhan (27), Richard Bora (33), Patrick Kwezi (26) l, Masood Salim (32), Revocuts Elaxanda (36) na Erick Daniel (28), wanadaiwa kufanya kosa la wizi kinyume na kifungu cha 258(1) na 265 cha sheria ya kanuni ya adhabu.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Johari Kijuwile, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Kabula Benjamen, ameieleza mahakama hiyo kuwa Julai 23,2023; washtakiwa hao kwa pamoja saa 3:30 usiku huko katika mgodi wa GGML, eneo la Loncon pit bila kuwa na kibali waliiba mawe kilo 54.1 yanayodhaniwa kuwa na dhahabu.

Alidai mahakamani hapo kuwa mawe hayo yanadhaniwa kuwa na dhahabu yenye wastani wa gramu 0.53 za dhahabu yenye thamani ya zaidi ya Sh 150,000 ambayo ni mali ya mgodi wa dhahabu wa Geita(GGML).

Washtakiwa hao wamekana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka umedai upelelezi haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Septemba 4, 2023 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa hao wako nje kwa dhamana baada ya kukidhi masharti yakuwa na mdhamini mmoja atakaesaini hati ya Sh300,000 pamoja na barua ya utambulisho kutoka kwenye eneo wanalotoka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live