Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sita kortini wakidaiwa kuvunja duka, kuiba mali za Sh31 milioni

Sita Kortiniii Bbbb.png Sita kortini wakidaiwa kuvunja duka, kuiba mali za Sh31 milioni

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu sita akiwemo Katibu wa Chama cha Wamiliki Ardhi na Nyumba Tanzania, Wilaya ya Temeke, Michael Kateka (68) wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kuvunja duka na kuiba vitu vyenye thamani ya zaidi ya Sh 31 milioni.

Mbali na Kateka, wengine ni Bilali Juma (32), mkazi wa Mtoni, Isiaka Kapemba (32), Hemed Kapemba(32), Fadhili Kapemba na mjumbe wa shina, Hassan Kitigi, wote wakazi wa Magurumbasi.

New Content Item (1)

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Nicas Kihemba alidai kati ya Novemba 2, 2022 maeneo ya Keko Makurumbasi, washtakiwa walivunja na kuingia kwenye duka la Isack Mtenga.

Pia anadaiwa siku hiyo waliiba vitu mbalimbali vya dukani ikiwemo tairi saba za gari, vioo vya gari vya scania, dawa za ng'ombe, nyaraka mbalimbali pamoja na spana moja ambavyo vina jumla ya thamani zaidi ya Sh31 milioni.

Washtakiwa walikana tuhuma hizo mbele ya mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ally Mkama.

Wakili Kihemba alida kuwa upelelezi umekamilka, hivyo kuiomba Mahakama ipange tarehe ya kuwasomea maelezo ya awali.

Washtakiwa wamepelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wenye barua zinazotambulika, mmoja atoe fedha taslimu Sh5 milioni au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo. Kesi itatajwa Machi 27, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live