Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sirro atua Kilindi kwenye mauaji ya watu watano

Kilindi Pc Data Sirro atua Kilindi kwenye mauaji ya watu watano

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku moja baada ya kutokea mauaji ya watu watano katika kijiji cha Elera wilayani Kilindi mkoani Tanga, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro amewasili katika eneo hilo.

Mauaji hayo hayo yalitokea jana Jumapili Januari 31, 2022 baada ya kuibuka mapigano kati ya wakulima na wafugaji.

Mashuhuda katika tukio hilo walidai kuwa watu hao watano walifariki dunia kwa kupigwa risasi na kukatwa mapanga.

Mkuu wa wilaya ya Kilindi (DC), Abel Busalama akiwa eneo la tukio jana alithibitisha vifo vya watu hao watano na watatu kujeruhiwa.

Busalama alizitaka pande zote mbili kusitisha mapigano na kusalimisha silaha zao ili utatuzi wa mgogoro huo ufanyike kwa njia ya amani kwani njia wanayotumiwa hawawezi kupata utatuzi.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewasili wilaya ya Busega mkoani Simiyu Kwaajili ya ziara kukagua, kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025.

Chongolo amewasili wailayan humo leo Jumatatu Januari 31, 2022 akiongozana na wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live