Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siro, Baba wa mfanyabiashara Mo Dewji wazungumza

22202 Baba+wa+mo+pic TanzaniaWeb

Sun, 14 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Siro aliliambia Mwananchi jana kuwa, polisi bado wanaendelea na upelelezi wa tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji, huku akiahidi kutoa taarifa zaidi leo.

Sirro aliyasema hayo alipokuwa kwenye maziko ya aliyekuwa mhasibu wa jeshi hilo, Arcado Nchinga yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

“Hapa niko msibani siwezi kuzungumza lolote, mambo ya upelelezi yana mahala pake. Naomba mnipe nafasi hadi kesho asubuhi,” alisema Sirro.

Kwa upande wake, baba wa mfanyabiashara huyo, Gulam Dewji Hussein alipotafutwa na Mwananchi kuzungumzia taarifa zozote kuhusu mwanaye, alisema familia ilikuwa haijapata chochote kutoka polisi hadi jana jioni.

Alipoulizwa kuhusu simu ya mwanaye inayosemekana ikipigwa inaita na kupokea ujumbe mfupi wa maandishi (sms), mzazi huyo alimtaka mwandishi wa habari hizi asubiri kwa kuwa muda huo (wa jioni) alikuwa na wageni na asingeweza kuzungumzia suala hilo. Hata alipotafutwa baadaye hakuweza kupatikana.

Chanzo: mwananchi.co.tz