Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sintofahamu Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake

Mbowe 1 3?fit=600%2C417&ssl=1 Sintofahamu Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu wametolewa katika chumba cha Mahakama na kupelekwa katika mahabusu iliyopo Mahakama hapa baada ya kuwepo kwa hali ya sintofahamu kutokana na utaratibu uliotangazwa Mahakamani na kupelekea kesi kuchelewa kuanza kusikilizwa.

Utaratibu mpya uliotangazwa Mahakamani leo ni kupunguza idadi ya wanaoingia ndani ya Mahakama kufuatilia kesi hiyo ambapo Mawakili walioruhusiwa ni 20, Waandishi wa Habari 10, Watu Maalum 3, Viongozi 5 na Ndugu 5.

Mabadiliko hayo yamefanya Jopo la Mawakili wa Freeman Mbowe kutoka nje ya chumba cha mahakama muda huu, kupinga Wafuasi wa CHADEMA na Watu wengine kuzuiwa kuingia mahakamani na Viongozi wa CHADEMA walioruhusiwa kugomewa kuingia na simu.

Mbowe na wenzake walifikishwa Mahakamani saa 4 kasoro ambapo hadi muda huu bado kesi haijaanza kusikilizwa mbele ya Jaji Mustafa Siyani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live