Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simulizi ya mama aliyeua mwanaye, akamkatakata vipande na kumchemsha

64089 Pic+simulizi

Mon, 24 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Wakati Polisi mkoani Geita wakimshikilia kwa uchunguzi Happyness Shedrack (36) anayedaiwa kumuua mtoto wake wa mwaka mmoja na nusu na kumkatakata vipande na kisha kuchemsha mabaki ya mwili wake jikoni, kiongozi wa kitongoji amesimulia jinsi tukio hilo lilivyokuwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Dismas Kissusi alisema jana wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ikiwamo kumfikisha mtuhumiwa hospitali kwa uchunguzi wa afya ya akili na matibabu.

Mwenyekiti Kitongoji cha Buligi, Manyonyi Manyonyi alisema Happyness alikuwa na matatizo ya akili na muda mwingi alikuwa chini ya uangalizi wa mama yake.

Hata hivyo, alisema siku ya tukio, mama yake alimwacha chini ya uangalizi wa mtoto wa miaka sita na mzazi wake huyo kwenda kumtafutia dawa.

“Mama huyo aliporejea alimkuta mtoto wake mwenye matatizo ya akili akiwa jikoni na alipoangalia alikuta chombo kilichoinjikwa jikoni kikiwa na vipande vya mwili wa binadamu,” alisema Manyonyi.

Mmoja wa ndugu wa mama huyo, Amon Mtani alisema katika familia hiyo yupo ndugu mwingine mwenye matatizo ya akili na kuiomba Serikali kuisaidia familia hiyo kwa kuwapatia tiba sahihi baada ya jitihada za muda mrefu za kuwatibu kushindikana.

Pia Soma

“Wote wawili (Happiness na ndugu yake) walianza kupata matatizo ya akili wakati mmoja, na mama yao amekuwa akihangaika bila mafanikio,” alisema Mtani.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya wakazi wa mji wa Geita walisema tukio hilo lililotokea katika Kijiji cha Buligi Ijumaa iliyopita, ni fundisho kwa jamii na Serikali kuchukua hatua ya kuwaweka chini ya uangalizi na ulinzi maalumu watu wenye dalili au matatizo ya akili ili kuepuka madhara kwa jamii.

Pamoja na kuhimiza ulinzi na uangalizi maalumu kwa wenye dalili za matatizo ya akili, John Sospeter na Lilian Alex walihusisha tukio hilo na imani za kishirikina walizodai zimeshamiri miongoni mwa wakazi wa Geita.

“Matukio mengi Geita yakiwemo ya ukatili ni matokeo ya watu kuwa na imani za kishirikina, kukosa hofu ya Mungu. Wengi hukimbilia kwa waganga hata kwa magonjwa yanayotibiwa kirahisi hospitali; madhara yake ni kama haya,” alisema Lilian.

Peter Camosage mkazi wa Kalangalala, alizitaka familia zenye wagonjwa wa akili kuwawekea ulinzi na kuwawahisha kwenye huduma za afya kuepuka madhara.

“Pamoja na vituo vya huduma ya afya kuhakikisha vinatibu wagonjwa baada ya vipimo badala ya mtindo uliozoeleka wa kutibu kwa mazoea, Serikali pia ihakikishe wagonjwa wenye matatizo ya akili wanawekwa eneo maalumu badala ya kuachwa wakiishi kwenye jamii na kusababisha mauaji kama haya,” alisema.

Mchungaji wa Kanisa la Lat Church of God la mjini Geita, Petro Abel alisema pamoja na uangalifu, Serikali inatakiwa kuhakikisha wagonjwa wenye matatizo ya akili wanapata matibabu bure kwenye vituo vyote vya huduma ya afya vya umma na binafs, kauli iliyoungwa mkono na Steven Bulata, aliyeiomba Serikali kumpa mtuhumiwa tiba sahihi.

Chanzo: mwananchi.co.tz