Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simbachawene ataka mwanaye ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria

Simbachawene Mwanaye Simbachawene ataka mwanaye ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria

Sun, 21 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amelitaka Jeshi la Polisi kumuadhibu mwanae kwa mujibu wa Sheria baada ya mwanae kuonesha jeuri ndani kituo cha Polisi baada ya kuvunja sheria za barabarani kwa kuendesha gari akiwa amelewa na kugonga mawili.

“Nimeiona clip inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii, nakiri kuwa huyo ni kijana wangu ambae ni mtu mzima anajitegemea na anafamilia yake.

Nimemwagiza Mkuu kituo kwa sababu amekosa adabu kwa jeshi la polisi na ametenda kosa la usalama barabarani ASHUGHULIKIWE BILA HURUMA KWA MUJIBU WA SHERIA.

Binafsi naomba radhi sana kwa walioathirika na mkasa huo lakini pia kwa jeshi la polisi na Watanzania wote.

POLENI KWA USUMBUFU WOWOTE MLIOUPATA” amesema Simbachawene.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live