Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siku tatu za Sabaya Jela

Video Archive
Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: wasafi Media

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ambaye kwa sasa ni Mfungwa wa miaka 30 jela amefikishwa mahakamani tena Leo katika kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha namba 27/2021 nayomkabili na wenzake sita.

Sabaya amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha majira ya Saa 3 asubuhi akiwa na wenzake huku yeye akiwa amenyolewa kipara.

Oktoba 15, 2021 Sabaya na Wenzake wawili kwenye kesi ya jinai namba 105/2021 walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya wizi na unyang'anyi wa kutumia silaha.

Chanzo: wasafi Media