Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sheria ya Makosa ya Mtandao ingetumika vizuri mahabusu zingejaa-Naibu Waziri

Handcuffs Sheria ya Makosa ya mtandao imekua ikilalamikiwa na watu wengi

Tue, 22 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kundo Mathew amesema kuna mkanganyiko kati ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA) kutokana na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015.

Mkanganyiko uliopo unawafanya Wananchi wanapokamatwa kwa makosa ya kimtandao kudhani wamekamatwa na TCRA. Amesema Sheria hiyo inasimamiwa na Jeshi la Polisi kupitia kwa Mkurugenzi wa Upelelezi (DCI).

Amesema Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 ingetumika kama inavyotakiwa, mahabusu zingejaa. Amewataka Polisi kutoa Elimu kwa kuwa mazingira yamebadilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live