Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sheria: Adhabu ya kosa la uhaini ni kifo

Slaa Mwambukusi Mdudeeee Sheria: Adhabu ya kosa la uhaini ni kifo

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vifungu vya 39 na 40 vya Sheria ya Kanuni za Adhabu vimeeleza matendo yanayoweza kutambulika kuwa ni makosa ya Uhaini pamoja na adhabu ya matendo hayo.

Vifungu hivyo vimeeleza mtuhumiwa anapokutwa na Hatia ya Uhaini adhabu yake ni Kifo.

Uhaini ni moja ya makosa makubwa ya Jinai kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni za Adhabu (Penal Code) Kifungu cha 39 (1).

Uhaini ni kosa la jinai . Ni kosa kati ya makosa makubwa ya jinai. Katika jinai yapo makosa makubwa na yapo makosa madogo.

Yumkini udogo na ukubwa wa kosa waweza kupimwa kwa kutizama adhabu ya kosa. Kosa ambalo huadhibiwa kwa adhabu ndogo huwa ni kosa dogo na lile ambalo huadhibiwa kwa adhabu kubwa huwa ni kosa kubwa.

1. NI SHERIA IPI HUELEZA MAKOSA YA JINAI. Sheria zinazofafanua makosa ya jinai zipo nyingi. Hakuna sheria moja katika makosa ya jinai. Hata hivyo sheria kuu katika makosa ya jinai ipo. Ni sheria inayojulikana kama kanuni za adhabu( penal code). Hii ni sheria kuu katika makosa ya jinai.

Ni sheria inayoeleza karibia makosa yote ya jinai. Mbali na sheria hiyo pia zipo sheria nyingine kama za kuzuia na kupambana na rushwa, sheria ya uhujumu uchumi, sheria ya ugaidi na nyinginezo. Hizi nazo hueleza makosa ya jinai.

Tofauti kubwa kati ya sheria hizi na ile ya kanuni za adhabu ni kuwa hizi sheria nyinginezo hueleza makosa rasmi ya jinai. Kwa mfano sheria ya ugaidi itaeleza mambo ya ugaidi tu na si vinginevyo, sheria ya uhujumu uchumi itaeleza makosa yanayotokana na uchumi tu na si vinginevyo, sheria ya utakatishaji fedha itaeleza utakatishaji fedha tu na si vinginevyo.

Wakati sheria ya kanuni za adhabu ndani mwake utakuta makosa tofauti tofauti ya jinai. Utakuta makosa ambayo hayafanani na yasiyokuwa na uhusiano.

Utakuta kuhusu kubaka, kuiba, kupigana, kuua, kuharibu mali, rushwa, kughushi , uhaini na mengine mengi. Kwahiyo kwa mtu anayehitaji kuyajua makosa ya jinai basi na asome sheria ya kanuni za adhabu.

2. UKIFANYA HAYA UTAKUWA UMETENDA UHAINI. (a) Kifungu cha 39 ( 1 ) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya muungano au popote akajaribu kumuua rais atakuwa ametenda uhaini.

(b) Pia mtu yeyote aliye ndani ya Jamhuri ya muungano au popote na akaanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya muungano atakuwa naye ametenda kosa la uhaini.

(c) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri, kuhusu kifo, kumlemaza, kumzuia, au kufungwa kwa rais atakuwa ametenda uhaini.

(d) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kumwondoa rais madarakani visivyo halali atakuwa ametenda uhaini.

(e) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kumwondolea rais heshima na jina la mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu, au kiongozi wa serikali atakuwa ametenda kosa la uhaini.

(f) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya muungano ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kupindua serikiali iliyo madarakani, kutishia serikali, bunge au mahakama atakuwa ametenda kosa la uhaini.

3. NI IPI ADHABU YA KOSA LA UHAINI. Vifungu vya 39 na 40 vya kanuni za adhabu ambavyo vimeeleza ni matendo gani yanaweza kuitwa uhaini vimeeleza pia adhabu ya matendo hayo. Vimeeleza kuwa adhabu ya kukutwa na hatia ya uhaini ni kifo. Uhaini ni kati ya makosa machache sana ambayo adhabu yake ni kifo.

Kwahiyo kwa namna yoyote ukijihusisha na tendo lolote kati ya matendo yaliyotajwa hapo juu ndipo utahesabika umetenda uhaini na adhabu yake ni kifo ikiwa itathibitika mahakamani. Kila kilichoelezwa hapo juu katika A – F ni tafsiri halisi ya uhaini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live