Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shehena vipodozi visivyoruhusiwa nchini mbaroni

RPC KYANDO Shehena vipodozi visivyoruhusiwa nchini mbaroni

Mon, 11 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JESHI la Polisi Mkoa wa Songwe limekamata shehena ya vipodozi vyenye viambata vya sumu maboksi 196 vilivyopigwa marufuku kuingia nchini.

Vipodozi hivyo vilikuwa vikiingizwa kwa njia ya magendo vikiwa na thamani ya Sh. milioni 98.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, George Kyando, alisema vipodozi hivyo vilikamatwa katika doria iliyofanyika usiku vikiwa kwenye gari T910 ABN aina ya Mitsubishi Canter ikitokea nchini Zambia na kuingia Tanzania kwa magendo.

Kamanda Kyando alisema kuwa ni matukio ya mwendelezo kwa shehena za vipodozi kukamatwa katika mpaka wa Tanzania na Zambia.

Kamanda Kyando alisema juzi usiku katika maeneo ya mtaa wa Kichangani kata ya Chapwa, tarafa ya Tunduma wilaya ya Momba, polisi wakiwa katika msako kwa kushirikiana na vyombo vingine za ulinzi na usalama, walikamata vipodozi aina mbalimbali katoni 199 ambavyo vimepigwa marufuku kuingia nchini.

Alisema mmiliki wa gari hajajitokeza na dereva aliyekuwa analiendesha alikimbia na kuwataka kujisalimishe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live