Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shamimu Mwasha na Mumewe jela maisha

D361f1dba9d021557676c8f8d78f2812 Shamimu Mwasha na Mumewe jela maisha

Wed, 31 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi (Mahakama ya Mafisadi), imewahukumu kifungo cha maisha Mfanyabiashara Abdu Nsembo na Mkewe Shamim Mwacha baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kusafirisha dawa za Kulevya aina ya Heroin.

Mahakama hiyo imetoa amri ya kutaifisha mali za wahukumiwa ikiwemo gari aina ya ‘Discover 4’ kuwa mali za Serikali, huku dawa hizo zikihitajika kutekezwa.

Katika kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2020, Hukumu imetolewa Jaji Elinaza Luvanda baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kati ya Jamhuri na Utetezi na kujiridhisha kwamba watuhumiwa wamekutwa na hatiani katika makosa mawili ya usafirishaji dawa za Kulevya.

Katika hukumu hiyo Jaji Luvanda amesema

“Ni kweli mshitakiwa namba 1 na namba 2 ni wakosaji wa kwanza na kama ilivyoelezwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi ni kwamba sheria imetoa adhabu kwa makosa haya.”

"Hivyo hakuna namna yoyote ya kutoa adhabu ya chini, katika kosa la kwanza wanahukumiwa kifungo cha maisha gerezani, pia katika kosa la pili pia wanahukumiwa hivyo hivyo kifungo cha maisha gerezani, hivyo adhabu mtatumikia kwa pamoja,"

Pia Jaji Luvanda amesema kielelezo namba 1 ambayo ni dawa za Kulevya kiteketezwe, kielelezo namba tano ambalo ni gari aina ya ‘Discover 4 Landrover’ kinataifishwa kuwa mali ya Serikali.

Chanzo: www.habarileo.co.tz