Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shamim, mumewe waendelea kusota rumande

97486 Shamim+pic Shamim, mumewe waendelea kusota rumande

Sat, 29 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Jalada la kesi inayomkabili mfanyabiashara Abdul Nsembo maarufu Abdukandida na mkewe, Shamim Mwasha limewasilishwa katika ofisi ya Taifa ya mashtaka.

Shamimu ambaye ni mmiliki wa Blog 8020 Fashion na mumewe wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 36/2019.

Washitakiwa hao ambao ni wakazi wa Mbezi Beach, Dar es Salaam  walifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 13, 2019.

Wakili wa Serikali mwandamizi,  Wankyo Simon amedai hayo leo Ijumaa Machi 28, 2020 mbele ya Hakimu Mkazi,  Vicky Mwaikambo wakati kesi hiyo ilipotajwa.

"Upelelezi wa shauri hili haujakamilika  jalada limewasilishwa katika ofisi ya Taifa ya mashtaka kwa ajili  kusomwa na kutolewa uamuzi wa kisheria,  hivyo tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa,” amedai wakili Wankyo

Hakimu Mwaikambo ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 13, 2020 kwa ajili ya kutajwa.

Pia Soma

Advertisement
Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanadaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride zenye uzito wa gramu 232.70

Ilidai kuwa Mei Mosi mwaka 2019 maeneo ya Mbezi Beach walisafirisha dawa za kulevya zenye uzito huo huku wakijua kufanya hivyo ni kosa  kisheria.

Chanzo: mwananchi.co.tz