Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shamba la Bangi Mtwara lateketezwa

Bangi 1 Abdulrahaman Bakari (42) akutwa na kilo 17 za bangi

Sat, 9 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi mkoani Mtwara wameteketeza shamba la bangi lenye ukubwa wa nusu hekari lililokuwa katika mtaa Rweru, kata ya Jangwani wilaya ya Mtwara mkoani humo.

Kaimu RPC Mtwara, Nicodemus Katembo amesema hatua hiyo imetokana na kukamatwa kwa Mtuhumiwa aitwaye Abdulrahaman Bakari (42) mkazi wa Mikindani akiwa amehifadhi bangi kiasi cha kilogramu 17 nyumbani kwake, marchi 27 mwaka huu na baada ya kufanya nae mahojiano ya kina alikiri kuwa yeye na ndugu yake aliyemtaja kwa jina la Himid Mohamed wanajishughulisha na kilimo cha bangi katika shamba la familia yao mtaa wa Rweru.

"Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea na mtuhumiwa mwingine aitwaye Himid Mohamed anatafutwa na Jeshi la Polisi na pindi upelelezi utakapokamilika watuhumiwa wote watakaobainika kuhusika kutenda kosa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live