Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi, wakili wakwamisha kesi ya Mpemba wa Magufuli

Shahidi, wakili wakwamisha kesi ya Mpemba wa Magufuli

Wed, 29 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kesi ya kukutwa na meno ya tembo inayomkabili, Yusuf Ali Yusuf maarufu Mpemba wa Magufuli na wenzake imekwama kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na shahidi kutofika mahakamani.

Washtakiwa wote katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 53/2016 wanakabiliwa na mashtaka manne, likiwemo la kujihusisha na mtandao wa ujangili.

Akizungumza leo Jumanne Januari 28, 2020 mahakamani hapo wakili wa Serikali, Slyvia Mitanto amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini shahidi waliyemtegemea hajafika.

Mbali na shahidi huyo kutofika, ilielezwa kuwa wakili anayeendesha shauri hilo naye amepata udhuru.

Baada ya maelezo hayo Hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 11,2020.

Mbali na Yusuph, washtakiwa wengine ni Charles Mrutu, Benedict Kungwa, Jumanne Chima, Ahmed Nyagongo na Pius Kulagwa.

Pia Soma

Advertisement

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manne, likiwemo la kujihusisha na mtandao wa ujangili.

Shtaka moja kati ya manne yanayowakabili ni kujihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za Serikali ambazo ni vipande 50 vya meno ya tembo vya Dola 180,000 za Marekani sawa na Sh392 milioni bila kuwa na kibali cha mkurugenzi wa wanyamapori.

Chanzo: mwananchi.co.tz