Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi wa tisa kesi vigogo TRL aeleza alivyokabidhi ripoti Takukuru

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ruben Mkuza, shahidi wa tisa katika kesi inayowakabili vigogo 11 wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ameieleza mahakama jinsi alivyokabidhi kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ripoti ya mchanganuo wa wajumbe watano wa bodi ya zabuni iliyochaguliwa na aliyekuwa mkurugenzi wa kampuni hiyo, Kipallo Kisamfu.

Vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kukiuka sheria katika ununuzi wa mabehewa 25 na leo Jumatano Mei 29, 2019 kesi yao imeendelea katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Shahidi huyo ambaye ni ofisa manunuzi mwandamizi wa  Shirika la Reli Tanzania (TRC) amedai mahakamani hapo kuwa  ripoti hiyo inaonyesha aliyeshinda zabuni hiyo ni kampuni ya Hindusthan Engineering Limited.

Akiongozwa na wakili wa Takukuru, Moghela Ndimbo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,  Huruma Shaidi, Mkuza amedai Aprili 19, 2016 akiwa kwenye majukumu yake ya kazi alipewa maelekezo kutoka kwa Kisamfu apeleke ripoti ya tathmini ya manunuzi ya aliyeshinda zabuni ya ununuzi wa mabehewa 25.

Mkuza amedai tarehe hiyo alipewa maelekezo kutoka kwa Kisamfu  amkabidhi ofisa wa Takukuru nyaraka za ripoti ya tathmini ya manunuzi ya kumpata mzabuni.

Amedai  ripoti hiyo ya wajumbe watano wa bodi ya zabuni ilichaguliwa na Kisamfu na kuwataja wajumbe hao kuwa ni mkuu wa kitengo cha makenika na mhasibu mkuu, Jasper Kisiraga; kaimu mhandisi wa mawasiliano, Felix Kashaingili; mhandisi wa mipango, Kedmo Mapunda; mkuu wa usafiri wa reli, Lowland Simtengu na kaimu mhandisi wa ufundi na meneja ujenzi, Andrew Kaupunda.

Pia Soma

Mkuza amedai kuwa zabuni aliyoshinda ya Kampuni ya Hindusthan Ingeneering Limited iliidhinishiwa malipo ya Dola za Kimarekani 2,561,187.50.

“Katika hati ya makabidhiano ya aliyesaini upande wa ofisa wa Takukuru alikuwa Victoria Nyarando na mimi na zabuni ni namba PA/113/2012/13/ME/G/0OE/013,”amedai Mkuza.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa kaimu meneja wa usafiri, Mathias Massae; mkuu wa ufundi na meneja ujenzi, Ngoso Ngosomwiles.

Mhandisi mkuu wa ufundi, Paschal Mafikiri; mkuu wa ubunifu na utengenezaji wa nyaraka, Joseph Syaizyagi na kaimu mkuu wa usafirishaji, Charles Ndenge.

Katika kesi ya msingi washtakiwa hao wanadaiwa kati ya Februari Mosi 2013 na Juni 30, 2014 makao makuu ya TRL, Kisamfu akiwa mfanyakazi wa mamlaka hiyo alitumia vibaya madaraka yake kwa kushindwa kusimamia vizuri zabuni kama ilivyokuwa inatakiwa kwenye vigezo na masharti.

Chanzo: mwananchi.co.tz