Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi wa tatu kesi ndogo ya Mbowe kutoa ushahidi leo

Mbowe 3?fit=600%2C350&ssl=1 Shahidi wa watatu kesi ndogo ya Mbowe kutoa ushahidi leo

Mon, 20 Sep 2021 Chanzo: mwananchidigital

Shahidi wa tatu katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ameanza kutoa ushahidi wake.

Shahidi huyo askari polisi mwenye namba H 4323 Constable Msemo kutoka Kituo Cha Polisi Oysterbay, ameanza kutoa ushahidi wake leo, Septemba 20, 2021 katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Shahidi huyo anaongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga, mbele ye Jaji Mustapha Siyani anayesikiliza shauri hilo.

Msemo anatoa ushahidi wake, baada ya shahidi wa pili katika kesi hiyo ndogo, Mkaguzi wa Jeshi la Polisi, Mahita Mahita kumaliza kutoa ushahidi wake na kisha kuhojiwa na mawakili wa upande wa utetezi kuhusiana na ushahidi alioutoa mahakamani hapo, kuhusiana na kielelezo kinachobishaniwa na upande wa utetezi.

Chanzo: mwananchidigital