Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi wa sita kutoa ushahidi leo kesi ya Mbowe

Mbowe Kesi 2 Pic Data Kesi ya akina Mbowe kuendelea leo, shahidi wa sita kutoa ushahidi

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake watatu wanaotuhumiwa kwa makosa ya ugaidi inatarajiwa kuendelea kuunguruma Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Alhamisi Novemba 4, 2021.

Mahakama hiyo leo inatarajiwa kuendelea kupokea ushahidi wa upande wa mashtaka kutoka kwa shahidi wa sita.

Kesi hiyo ilishindwa kuendelea jana baada ya shahidi aliyekuwa ameandaliwa kushindwa kufika mahakamani kutokana na kuugua.

Tayari washtakiwa wameshafikishwa kwenye chumba cha mahakama na Mawakili wa pande zote pia wameshafika mahakamani mpaka sasa ni Jaji Joachim Tiganga ndiye anayesubiriwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live