Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi wa saba kutoa ushahidi kesi ya kina Mbowe leo

Shahidipic Wasaba Shahidi wa saba kutoa ushahidi kesi ya kina Mbowe leo

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Kesi ya uhujumu uchumi na ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu inaendelea kusikilizwa leo Ijumaa November 5, 2021 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Katika muendelezo wa kesi hiyo leo shahidi wa saba wa upande wa Jamhuri anatarajiwa kuanza kutoa ushahidi.

Mbali na Mbowe washtakiwa wengine ni Halfani Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa maarufu kama Adamoo na Mohamed Abdillahi Ling'wenya ambao walikuwa makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko 92 KJ Ngerengere, wanaodaiwa kuachishwa kazi kwa sababu za kinidhamu.

Wote wanakabiliwa na mashtaka sita, likiwamo la kula njama kufanya ugaidi na kutishia amani na usalama kwa lengo la kusababisha hofu kwa wananchi wa Tanzania na kupanga kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Wanakabiliwa na mashtaka sita ya vitendo vya kigaidi, kama vile mipango ya kulipua vituo mbalimbali vya mafuta katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya, kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na kuziba barabara kwa kuweka miti.

Chanzo: mwananchidigital