Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi wa nne kutoa ushahidi kesi ya Mbowe na wenzake leo

Mbowe Kesi 2 Pic Data Freeman Aikael Mbowe, Mwenyeketi wa CHADEMA

Mon, 1 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, wanaokabiliwa na mashtaka ya ugaidi inaendelea kusikiliza leo Novemba Mosi, 2021 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Katika muendeleozo wa kesi hiyo, leo shahidi wa nne wa upande wa mashtaka anatarajiwa kutoa ushahidi.

Tayari mawakili wa upande wa utetezi wameshaingia kwenye chumba cha mahakama wakaisubiri washtakiwa kuletwa.

Hivi sasa washtakiwa wamefikishwa mahakamani na baada ya kushushwa kwenye gari la Jeshi la Magereza lililokuwa limewabeba, wamingizwa katika mahabusu ya Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi wakisubiri kupandishwa kizimbani kuendelea na usikilizwaji wa kesi yao.

Endelea kufatilia TanzaniaWeb kwa taarifa zaidi kuhusu kesi hii

Chanzo: www.tanzaniaweb.live