Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi wa Sabaya akiri kumiliki simu

F7a0a33c4b7abc1b875030f3e448350f Shahidi wa Sabaya akiri kumiliki simu

Tue, 8 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SHAIDI wa tatu katika kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro,Lengai Ole Sabaya{35} na wenzake sita, Enock Mnkeni[41} amekiri kumiliki simu ya kiganjani yenye namba 0759 978686 iliyosajiwa kwa jina lake kuwasiliana mara kwa mara na simu namba 0758 707171 iliyosajiLiwa kwa jina la Lengai Ole Sabaya januari 22 mwaka jana katika maeneo mbali mbali mkoani Arusha na Kilimanjaro.

Mnkeni, ambaye ni mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo alijitetea wakati akihojiwa na Mwendesha Mashitaka Mwandamizi wa Serikali Tasila Asenga mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha,Patricia Kisinda.

Akihojiwa na Asenga kuwa kama ana utaalamu wowote wa kielektroniki wa kutambua ama kujua CCTV Camera zinapofanya kazi shahidi huyo alidai kutojua hilo.

Asenga alimkabidhi kielelezo P3 taarifa ya mawasiliano kutoka kampuni ya Vodacom ikionyesha mawasiliano ya simu yake 0759 978686 iliyosajiriwa kwa jina lake ikiwa inawasiliana mara kwa mara na namba ya simu 0758 707171 iliyosajiriwa kwa jina la Lengai Ole Sabaya siku ya januari 22 mwaka jana na kukiri kuwasiliana na simu hiyo siku hiyo lakini kwa biashara ya mazao na aliyekuwa akiongea alikuwa mwanamke.

Pia aliambiwa kusoma kielelezo P3 siku hiyo ya januari 22 mwaka jana majira ya saa 4;0;43 asubuhi kinaonyesha alikuwa wapi na aliposoma kielelezo hicho aliiambia Mahakama kuwa siku hiyo mnara wa Voda ulionyesha alikuwa Boma ya Ng’ombe Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.

Mbali ya Sabaya washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni pamoja na Enock Mnkeni (41),Watson Mwahomange (27) maarufu kwa jina la Malingumu, John Aweyo (45), Syliverster Nyegu {26} maarufu kwa jina la Kicheche ambaye pia ni msaidizi wa Sabaya, Jackson Macha (29) na Nathan Msuya(31).

Wakati huo huo shahidi wa 4 katika kesi hiyo ambaye ni mshitakiwa wa 4,John Aweyo{49} amedai kuwa hamjui wala hamfahamu Sabaya na washitakiwa wengine katika kesi hiyo kwani kwa mara ya kwanza amekutana nao Mahakamani na wengine Gerezani Kisongo Arusha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live