Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi mwingine kesi ya Sabaya kujitetea leo

71fcba41b643aa31469323189aecaa99.jpeg Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shahidi wa nne upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya {35} na wenzake sita leo anatarajiwa kutoa ushahidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha.

Kesi hiyo ilihairishwa mwezi uliopita kwa kuwa jopo la waendesha mashitaka wa serikali walikuwa kwenye semina ya kuongeza weledi katika utendaji kazi.

Shahidi huyo ni mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo Enock Mnkeni (41) na anatarajiwa kujitetea mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha, Patricia Kisinda.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Watson Mwahomange {27}, John Aweyo 45), Syliverster Nyegu {26}, Jackson Macha {29} na Nathan Msuya {31}.

Shitaka la kwanza linaliwakabili washitakiwa wote ikidaiwa kuwa Januari 20 mwaka huu ndani ya Jiji la Arusha Sabaya akiwa na genge la uhalifu alilokuwa akiliongoza alitumia vibaya madaraka yakje akiwa Mkuu wa Wilaya.

Shitaka la pili linamkabili Sabaya akidaiwa kuwa Januari 20 mwaka huu ndani ya Jiji la Arusha na Mkoa wa Arusha alishiriki kuomba rushwa ya shilingi milioni 90 kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mrosso.

Katika shitaka la tatu Sabaya anadaiwa kuomba rushwa ya shilingi milioni 90 kwa Mrosso ili aweze kumsaidia katika kesi ya jinai ya ukwepaji kodi iliyokuwa ikimkabili.

Shitaka la nne linamkabili Sabaya akidaiwa kuwa Januari 20 mwaka huu ndani ya Jiji la Arusha na Mkoa wa Arusha aliomba rushwa ya shilingi milioni 90 kutoka kwa Mrosso.

Katika shitaka la tano la utakatishaji fedha haramu ilidaiwa kuwa Januari 20 mwaka huu ndani ya Jiji la Arusha na mkoa huo ilidaiwa kuwa washitakiwa wote walichukuashilingi milioni 90 kwa Mrosso na kwenda kuzifanyia matumizi yasiyokuwa halali kinyume na sheria ya utakatishaji fedha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live