Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi kesi ya Lucky Vicent asema bima ya gari lililopata ajali ilikuwa batili

42057 Lucky+pic Shahidi kesi ya Lucky Vicent asema bima ya gari lililopata ajali ilikuwa batili

Mon, 18 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Shahidi wa tano katika kesi ya ajali iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa gari la Shule ya Lucky Vincent, Mahmudu Saidi (37) amesema gari lililopata ajali bima yake ilikuwa batili.

Akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya mkoa Arusha, Niku Mwakatobe leo Ijumaa Februari 15, 2019 amesema gari hilo lilikuwa likituma bima yenye jina la Swalehe Sadiki aliyekuwa akimiliki gari hilo ambalo tayari alikuwa amewauzia uongozi wa Shule ya Lucky Vincent.

Shahidi huyo amesema ni kosa kutokurudisha bima aliyokuwa akiitumia katika gari hilo na mmiliki wa awali.

Shahidi huyo, akiongozwa na mawakili wa Serikali Judith Sekule, amesema inapotokea ajali bima ambayo inasomeka kwenye gari ndiyo ambayo hutumika na hivyo ilipaswa baada ya gari hilo kuuzwa ikatwe bima nyingine ya mmiliki mpya.

Mahamudu amesema pia kama athari zitatokea endapo mmiliki wa gari atauza bila kutoa taarifa hupelekea mmilikiakukosa haki zake za bima.

Wakili wa upande wa utetezi Method Kimomogo akimhoji shahidi huyo, ameomba barua iliyotoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (TRO) kwenda katika kampuni ya Zanzibar Insurance na kutaka kujua kampuni hiyo ilijibu nini baada ya kutakiwa kutolea ufafanuzi suala hilo.

Shahidi huyo amejibu kuwa kama mmiliki ameuza gari alipaswa kuondoa bima na kama iliendelea kutumika kwa mmiliki mwingine si sahihi.

Wakili wa Serikali Judith Sekule amemuuliza swali shahidi huyo kuwa ni kwa wakati gani kampuni ya bima inatakiwa kubadilisha bima ambapo shahidi huyo kila anapopatikana mmiliki mpya anapaswa kuripoti kampuni ya bima na kurekebisha bima yake.

Kesi hiyo, iliahirishwa hadi Februari 21, 2019 ambapo dhamana ya washtakiwa bado inaendelea.

Katika kesi hiyo, mmiliki wa shule hiyo Innocent Moshi na mwalimu mkuu msaidizi, wanakabiliwa na makosa matano tofauti, kutokana na ajali hiyo, ambayo ilitokea katika mteremko wa Mlima Rhotia, wilayani Karatu Mei 6 mwaka 2017.

Mmiliki wa shule hiyo ana mashitaka manne, kufanya biashara ya usafirishaji abiria bila kuwa na leseni, kuruhusu gari kutumika bila kuwa na bima pamoja na kushindwa kuingia mkataba na dereva mwajiriwa wake na kuzidisha abiria 13 katika basi lililopata ajali.

Makamu mkuu wa shule hiyo, Nkana anakabiliwa na shitaka moja la kuzidisha abiria 13 katika gari lililobeba wanafunzi ambalo lilipata ajali.



Chanzo: mwananchi.co.tz