Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi kesi ya Dk Pima augua

Md Pima Shahidi kesi ya Dk Pima augua

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: mwanachidigital

Kesi ya uhujumu uchumi namba 5/2022 inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili imeshindwa kuendelea, baada ya shahidi wa Jamhuri kudai bado anaumwa.

Mbali na Dk Pima watumiwa wengine ni aliyekuwa Mwekahazina wa jiji hilo, Mariam Mshana na aliyekuwa mchumi Innocent Maduhu, ambao kwa pamoja wanakabiliwa na makosa tisa ikiwemo utakatishaji fedha Sh 103 milioni.

Leo Ijumaa Februari 17, 2023 shahidi wa 22 wa Jamhuri alitarajiwa kuanza kutoa ushahidi wake, lakini wakili wa Serikali mwandamizi, Hebel Kihaka ameiomba Mahakama iahirishe kesi hadi Februari 20, 2023 kwa kuwa shahidi ana udhuru wa kiafaya.

"Tunaomba iahirishwe kwa leo ili tuendelee na shauri hili Jumatatu na tunaomba kuanza saa nne asubuhi, kwani tutakuwa Mahakama Kuu katika shauri lingine la rufaa namba 155/2022 mbele ya Jaji Salma Maghimbi," amesema.

Leo Jamhuri iliwakilishwa na mawakili wa Serikali waandamizi Kihaka, Timotheo Mmari na wakili wa Serikali Nickson Shayo huku utetezi wakiwakilishwa na mawakili Mosses Mahuna na Fridolin Bwemelo.

Hakimu Mkazi Serafini Nsana anayesikiliza kesi hiyo alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hadi Februari 20, 2023.

Hadi sasa mashahidi 21 na vielelezo 24 vya Jamhuri vimeshawasilishwa mahakamani hapo ambapo katika kesi hiyo watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa tisa ikiwemo utakatishaji Sh 103 milioni.

Chanzo: mwanachidigital