Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi ataja fedha za Malinzi Stanbic

56043 Pic+malinzi

Tue, 7 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shahidi wa 18 katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake wanne, ameieleza mahakama namna fedha taslimu na dola zilizokuwa zikitoka TFF na kuwekwa kwenye akaunti binafsi ya Malinzi.

Shahidi Joan Mbise ambaye ni Meneja Uhusiano wa Akaunti Binafsi wa Benki ya Stanbic alitoa ushahidi mbele ya Hakimu, Maila Kasonde akiongozwa na Wakili wa Takukuru, Leonard Swai.

Mbise alidai Malinzi alikuwa na akaunti mbili katika benki hiyo yenye fedha za Kitanzania na dola na waliokuwa wakiweka fedha hizo ni Hellen Adam, dereva wake, Steven Mgunda na Malinzi .

Alidai kuanzia Januari hadi Desemba 2016 kwenye akaunti ya fedha taslimu inawaonyesha Hellen na Steven kila mmoja aliweka zaidi ya Sh30 milioni kwenye akaunti ya Malinzi. Mbise aliiomba mahakama hiyo kuvipokea vielelezo hivyo vitumike katika ushahidi wake.

Wakili wa utetezi, Abrahamu Senguji alidai ushahidi unaenda taratibu na wana uhakika mashahidi walioandaliwa wapo nchini, hivyo aliiomba mahakama iwaeleze upande wa mashtaka kuwaleta mashahidi wote mahakamani.

Hakimu Kasonde aliahirisha shauri hilo hadi Mei 20, 2019 na ameutaka upande wa mashataka kuhakikisha mashahidi walioandaliwa wanafika siku ya shauri hilo.



Chanzo: mwananchi.co.tz