Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi ashangaa walinzi wa Sabaya kutoshitakiwa

D29dd2690c20a429c0a7b7830476223f Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya HAI, Ole Sabaya

Tue, 3 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SHAHIDI wa sita katika kesi inayowakabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ha mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, Bakari Msangi {38} ameshangaa baadhi ya walinzi wa Sabaya kutoshitakiwa.

Katika kesi hiyo, Sabaya na wenzake, Silverster Nyengu [26} na Daniel Mbura {38} wanadaiwa walitumia silaha Februari 9 mwaka huu kupora mali na fedha Sh milioni 3,159,000 katika duka la Shahiid Store lililopo Mtaa wa Bondeni jijini Arusha.

Wakati akihojiwa na wakili Edmund Ngemela anayemtetea mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo mbele ya Hakimu Mwandamizi Odira Amworo katika Mahakama ya Hakimu Mkadhi Mkoa wa Arusha, Msangi alisema walinzi wa Sabaya, Deogratusi Peter na mlinzi mwingine aliyemtambua kwa jina moja la Andwer ni miongoni mwa walinzi wa Sabaya na waliohusika kumpiga hadi akapoteza fahamu.

Wakati akihojiwa na wakili Fridolin Gwemelo anayemtetea mshitakiwa wa tatu, Msangi alisema alimtambua Sabaya, Silvester Hajirini, Norman na kwamba hakuwatambua walinzi wengine kwa sababu walivaa kofia zilizoficha sura zao na walikuwa zaidi ya 10.

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano katika ya wakili Gwamelo na Msangi:

Wakili; Hapa Mahakamani ulisema kuwa ulipofika dukani siku ya tukio uliwatambua Sabaya na Silvester ni kweli?

Shahidi: Nilisema nilimtambua Sabaya, Silvester, Hajirini na Norman na walinzi wengine wa Sabaya sikuwatambua kwa sababu walivaa kofia (kapelo) iliyochifa uso

Wakili: Ulisema walinzi walivua kofia?

Shahidi: Nilisema walivua kofia wakati walipokuwa katika Kituo cha Mafuta cha Panoni Wakili: Uliandika maelezo polisi? Shahidi:- Ndio.

Wakili: Ulindika maelezo Polisi tarehe 10/2/2021 ?

Shahidi: Ndio.

Wakili: Ni kweli yalikuwa maelezo ya tukio la tarehe 9/2/2021? Shahidi: Ndio. Wakili: Katika maelezo ya polisi ulimtaja Mbura na Silvester ?

Shahidi: Katika maelezo yangu ya siku tatu hapa mahakamani nilisema na kumtamka Mbura na Silvester.

Wakili: Wakati uko Tulia Lodge ulichukua simu yako ya mkononi na kumpigia simu mke wako?

Shahidi: Si kweli kwa sababu nilifungwa pingu mkononi hivyo sikuweza kufanya hivyo.

Wakili: Katika maelezo yako Polisi uliandika kumtambua Sabaya na Andwer ni kweli?

Shahidi: Si Kweli. Wakili: Katika maelezo yako Polisi ulisema Sabaya na wenzake walikuwa na bunduki mbili ni kweli?

Shahidi: Hapana walikuwa na bunduki saba.

Wakili: Polisi ulisema ulinyang’anywa pochi na Sh 390,000?

Shahidi: Hapa nilisema niliporwa Sh 390,000.

Wakili: Ni kweli Polisi ulisema Sabaya alikuambia kuwa wewe unasaidia Al Qaida?

Shahidi: Hapana nilisema Alswan Sunny.

Wakili: Katika maelezo yako ya nyongeza Polisi, ulitaja majina ya watu uliowatambua? Shahidi: Nilitajiwa na polisi kuwa wale niliowatambua katika gwaride ni Mbura na Peter.

Wakili: Ntakuwa sahihi nikisema uliandika maelezo yako polisi baada ya tarehe 10/2/2021?

Shahidi: Niliandika maelezo yangu tarehe 10/2/2021 na tarehe 16/2/2021.

Wakili: Nikuonesha maelezo yako unaweza kuyatambua? Shahidi: Ni kweli nitayatambua kwa sababu nilisaini na saini yangu sijui kama kuna mtu anaweza kuigushi.

Wakili: Angalia, haya ni maelezo yako uliyoyatoa polisi na yenye saini yako? Shahidi: Ni kweli ni maelezo yangu na yana saini yangu ila page {karatasi} zilikuwa zaidi ya kumi hapa zimepungua karatasi nne na sijui ziko wapi?

Chanzo: www.habarileo.co.tz