Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi apandishwa kizimbani kwa kuidanganya mahakama

Shahidi Mwananchi Shahidi apandishwa kizimbani kwa kuidanganya mahakama

Fri, 7 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Magomeni Mwembechai, Mwanamtama Sasamalo (56) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kujibu shtaka moja la kutoa ushahidi wa uongo mahakamani.

Sasamalo amefikishwa mahakamani hapo, leo Juni 7, 2024 na kusomewa kesi ya jinai namba 15462 ya mwaka 2024.

Mshtakiwa huyo amesomewa shtaka lake na Wakili wa Serikali Erick Kamala mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Gwantwa Mwankuga.

Akimsomea shtaka hilo, Kamala amedai Juni 4, 2024 katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa shahidi wa upande wa Jamhuri, alitoa ushahidi wa uongo kwa ni ya kuipotosha Mahakama.

Sasamalo baada ya kusomewa shtaka linalomkabili, amekana kutenda kosa hilo na upande ea mashtaka umedai upelelezi wa shauri hilo unaendelea, hivyo unaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mwankuga amesema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi, akitakiwa awe na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria, watakaosaini bondi ya Sh2 milioni kila mmoja.

Mshtakiwa ametimiza masharti ya dhamana na kuachiwa kwa dhamana, hadi Julai 3, 2024 kesi itakapotajwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live