Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi akwamisha kesi ya bosi Jamii Forum

Fri, 19 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kesi ya kuendesha mtandao ambao haujasajiliwa Tanzania kwa kikoa cha co .tz (Tanzania domain) inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo na mwenzake Micke William imeshindwa kuendelea na ushahidi katika Mahakamaya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kesi hiyo ya Jinai namba  458 ya mwaka 2016 ilipaswa kuendelea na ushahidi leo Alhamisi Aprili 18, 2019 lakini upande wa mashtaka hawakuwa na shahidi.

Wakili wa Serikali, Jenifa Masue amedai mbele ya Hakimu Mkazi Agustino Mmbando kuwa, kesi hiyo ilikwenda mahakamani kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini upande wa Jamhuri hawana shahidi hivyo kuomba tarehe nyingine.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Mmbando ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 9 itakapoendelea na ushahidi.

Katika kesi hiyo, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Desemba 9, 2011 na Desemba 13, 2016 maeneo ya Mikocheni, wilaya ya Kinondoni.

Washtakiwa  wanadaiwa kuendesha mtandao ambao haujasajiliwa nchini na kushindwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kuzuia taarifa binafsi za wateja wa mtandao huo.

 Soma zaidi>> Wakili akwamisha Kesi ya Jamii Forum

>>Bosi Jamiiforums aenda rumande



Chanzo: mwananchi.co.tz