Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi akwamisha kesi ya Maxence Melo

72994 Pic+melo

Mon, 26 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Kesi ya kuendesha mtandao ambao haujasajiliwa nchini Tanzania kwa kikoa cha .co .tz (Tanzania domain) inayomkabili, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo na mwenzake Micke William, imeshindwa kuendelea na ushahidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Kesi hiyo ya Jinai namba  458 ya mwaka 2016, ilipaswa kuendelea na ushahidi, lakini upande wa mashtaka hawakuwa na shahidi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Saimon amedai leo Jumatatu Agosti 26, 2019 kuwa kesi hiyo imekuja kwaajili ya kuendelea kusikilizwa lakini shahidi waliomtegemea hayupo na kuomba tarehe nyingine.

"Kesi imekuja kwaajili ya kuendelea na ushahidi lakini shahidi tuliyekuwa tunamtegemea Esther Tully Mwambapa kutoka CRDB hayupo hivyo tunaomba ahirisho kwa mara ya mwisho," amedai Wakili Wankyo.

Kutokana na maelezo hayo,  Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma  Shahidi aliutaka upande wa mashtaka kuleta mashahidi mahakamani hapo ili kesi hiyo iweze kumalizika.

Hakimu Shahidi, ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba Mosi, 2019 itakapoendelea na ushahidi.

Pia Soma

Katika Kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Desemba 9, 2011 na Desemba 13, 2016 katika eneo la Mikocheni, wilaya ya Kinondoni.

Washtakiwa  wanadaiwa kuendesha mtandao ambayo haujasajiliwa nchini, yaani .tz (Tanzania domain) na kushindwa 'kutoa ushirikiano' kwa Jeshi la Polisi kwa kuzuia taarifa binafsi za wateja wa mtandao wake.

SOMA ZAIDI

> Mkurugenzi Jamii Forums ashinda tuzo ya kimataifa ya uhuru wa habari

> Kesi ya mabosi Jamii Forum yakwama

Chanzo: mwananchi.co.tz