Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi akwamisha kesi mtihani darasa la saba

Hukumu Pc Data Shahidi akwamisha kesi mtihani darasa la saba

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Upande wa mashtaka katika kesi ya kusambaza mtihani ya Taifa ya darasa la saba kwa njia mtandao wa kijamii wa ‘telegram,’ umeshindwa kumfikisha shahidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa kile ulichodai “kuchanganya tarehe za shauri.”

Wakili wa Serikali, Aroun Titus ameiambia mahakama hiyo kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini leo hawakumleta shahidi kwa kuwa walijua shauri hilo limepangwa kesho Alhamisi Oktoba 12 na 13, 2023.

"Tumechanganya tarehe, tulijua shauri hili litakuja Oktoba 12 na 13, 2023 ambapo tuliandaa shahidi aweze kutoa ushahidi wake, naiomba mahakama hii ipange tarehe ya kesho," alidai Titus.

Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo ameahirisha shauri hilo hadi Oktoba 12, 2023 kwa ajili ya usikilizwaji ambapo watu 12 wakiwemo walimu, wanakabiriwa kesi ya kesi ya kusambaza mtihani ya Taifa ya darasa la saba kwa njia mtandao wa kijamii wa ‘telegram.

Wanaokabiliwa na kesi hiyo ni pamoja na Jahnson Ondieka, Patrick Chawawa, Theresia Chitanda, Elinami Sarakikya, Joyce Nyanyakila, Gladius Roman, Lioyd Mpande, Ronald Odongo, Dorcas Muro, Alcheraus Malinzi, Jacob Adagio na Joel Ngome.

Katika kesi ya msingi, inadaiwa kuwa kati ya Oktoba 2, 2022 na Oktoba 12, 2022 sehemu isiyojulikana washtakiwa hao walitengeneza nyaraka za uongo za mitihani ya masomo ya Uraia na Maarifa ya Jamii ya darasa la saba, wakijifanya mitihani hiyo ni halali na imeandaliwa na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta).

Pia katika tarehe hizo na maeneo yasiyojulikana, washtakiwa hao walivujisha mitihani ya Taifa ya darasa la saba kinyume cha sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live