Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi aeleza alivyopigwa jiwe mkononi na kichwani, wakati akizuia maandamano ya wafuasi wa Chadema

60762 Pic+mbowe

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar Es Salaam. Shahidi wa nne, katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe,  ameieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi alivyopigwa jiwe kichwani na kupelekea kuvuja damu nyingi.

Shahidi huyo, ambaye ni askari Polisi wenye namba H 7856 PC Fikiri Mgeta kutoka kituo cha Polisi Oysterbay  ameeleza hayo leo, Mei 31, 2019, wakati akitoa ushahidi wake dhidi ya viongozi hao wa Chadema.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Jackline Nyantori, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, shahidi huyo alidai kuwa Februari 16, 2018 aliingia kazini akiwa na wenzake na alipangiwa kufanya doria katika eneo la Mwananyama  wilaya Kinondoni.

" Ilipofika saa  11 hadi 12 jioni, nilipewa taarifa na kiongozi wangu wa doria, Sajenti Hamad kuwa tunahitajika kwenda Mkwajuni ambapo kulikuwa kuna mkusanyiko wa watu waliokuwa wanatishia amani" alidai shahidi.

Alidai kuwa walipofika Mkwajuni walikuta barabara zote zimefungwa na  watu wanaodaiwa  kuwa ni waandamanaji wa viongozi wa Chadema huku wakiiomba nyimbo ' Hatupoi, hatuogopi bunduki watatuua'.

Amedai walipofika eneo hilo, Mkuu wa oparesheni mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Gerald Ngichi alitoa ilani ya kuwataka wafuasi hao kuondoka eneo hilo lakini walikaidi.

Pia Soma

" Baada ya waandamanaji hao kushindwa kutii tamko la ilani la  kutawanyika, askari wenye mabomu ya machozi walisonga mbele kwa ajili ya kutumia mabomu kwa lengo la  kutawanya waandamanaji waliokuwa wameandamana" amedai Mtega.

Amedai kuwa mabomu ya machozi yalipigwa lakini kwa bahati mbaya, waandamanaji hao hawakukimbia bali waliendelea kusonga mbele huku viongozi wa Chadema wakiendelea kuhamasisha wafuasi wao kutupa mawe  upande wa askari.

"Katika hali hiyo, askari Rahim alianguka chini baada ya kupigwa  jiwe shingoni" Amedai Mtega

Shahidi huyo, amedia wakati askari mwenzake akipigwa jiwe mkono wa kulia na kupelekea  kupoteza saa  yake.

 

"Pia, wakati nahamaki jiwe nililopigwa katika mkono wa kulia, nilipigwa tena jiwe jingine kichwani na jiwe hilo lilitokea upande wa waandamanaji hali iliyopelekea nivuje damu nyingi na kupelekwa katika hospitali ya Polisi ya Kilwa kwa ajili ya matibabu" Amedai Shahidi.

Mgeta amedai kuwa baada ya kufikishwa hospitali ni hapo, alilazwa kwa siku mbili kuanzia Februari 16 , 2018 hadi Februari 18, 2018 aliporuhusiwa kutoka hospitalini  hapo kutokana na hali yake kuimarika.

Mbali na Mbowe, washitakiwa wengine katika kesi hiyo, ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vicenti Mashinji; naibu katibu mkuu wa chama hicho Salum Mwalimu na John Mnyika Mwenyekiti wa baraza la wanawake , Halima Mdee.

Wengine, ni Ester Bulaya mbunge wa Bunda, Mchungaji Peter Msigwa, mbunge wa Iringa Mjini na John Heche, mbunge wa Tarime Vijijini.

Mbowe na viongozi wengine wanakabiliwa na mashtaka 13 ya uchochezi, ikiwemo kuhamasisha wafuasi wao kutenda makosa, na kufanya mkusanyiko usio halali.

Chanzo: mwananchi.co.tz