Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh70 milioni zawapeleka jela Simanjiro

Hukumu Pc Data Sh70 milioni zawapeleka jela Simanjiro

Sun, 25 Jun 2023 Chanzo: Mwananchi

Mahakama ya wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, imewahukumu watu wawili kwenda jela kwa kosa la wizi wamali na fedha vyenye thamani ya Sh70 milioni.

Dhahma hiyo imemkuta Juma Athuman (23) mkazi wa Naisinyai wilayani Simanjiro ambaye amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitano huku Pili Mariam Mbega (26) mkazi wa Tabata jijini Dar es salaam akihukumia kutumikia kifungo cha mwaka mmoja. Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, Onesmo Nicodemo ametoa hukumu hiyo kwa wawili hao kwenye kesi namba 100/2023.

Hakimu Nicodemo amesema kwa kosa la kuvunja, Athuman amehukumiwa miaka mitano, na kwa kosa la wizi wa fedha Sh70 milioni, Mahakama amehukumu adhabu ya miaka mitatu, na kwamba kwa kosa la wizi wa Sh3 milioni amehukumiwa mwaka mmoja. Kwa mujibu wa hakimu huyo, Athuman pia atatumikia kifungo cha mwaka mmoja kwa kukutwa na mali ya wizi, hata hivyo, vifungo hivyo vitatumikiwa sambamba na hivyo kufanya adhabu hiyo kuwa ya miaka mitano jela. Kwa upande wa Pili, yeye amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na mali ya wizi na fedha Sh3 milioni. Hakimu Nicodemo amesema Athumani na Pili walifanya matukio hayo Juni 6 mwaka 2023 mji mdogo wa Mirerani. Awali katika kuirahisishia Mahakama kazi, washtakiwa hao walikiri makosa yao walipoulizwa na Hakimu Nicodemu mahakamani hapo. Hakimu Nicodemu ametoa amri kuwa fedha zilizopo benki Sh47 milioni zitolewe na kwamba Sh44 milioni arudishie Lawrent Elias huku kiasi kilichobaki cha Sh3 milioni arudishiwe John Simon.

Chanzo: Mwananchi