Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh535 milioni za Uviko-19 zamaliza tatizo la maji kaya 8,000 Rungwe

Kayapiic Data Sh535 milioni za Uviko-19 zamaliza tatizo la maji kaya 8,000 Rungwe

Sat, 10 Sep 2022 Chanzo: Mwananchi

Zaidi ya Kaya 8,356 katika Kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe, Mbeya zimeanza kunufaika na mradi wa maji wenye thamani ya Sh535 millioni unaozalisha lita 19,000 kwa siku kupitia fedha za Uviko 19.

Akizungumza leo Jumamosi, Septemba 10,2022, baada ya kukagua na kuzindua tanki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi  lita 135,000, kiongozi wa  Mbio za Mwenge Kitaifa 2022, Sahili Nyazabara amesema miradi  inayotekelezwa na Wakala wa Maji Vijijini (Ruwasa) ni fursa kwa wananchi kuunganishiwa huduma hiyo muhimu.

Tanki hilo lililozinduliwa na Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi linatarajiwa kusambaza maji katika vituo 16 vilivyosambazwa katika maeneo ya vijiji vinavyozunguka eneo hilo.

''Leo Mwenge tunazindua mradi huu, sasa niwasihi tu wateja ambao watapata maji wawe wepesi kulipia ankara za matumizi. Nina taarifa kuna wananchi huwa wanagoma kwa madai kwamba maji yameletwa na Mungu,” Nyazabara amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dk Vincent Anney amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia jamii kupata huduma bora na kuchochea shughuli za kiuchumi hususan kilimo cha mbogamboga.

Naibu Waziri Mahundi amesema, “Ndugu zangu mmeona fedha zilizotolewa na Serikali ni nyingi katika kutekeleza mradi huu, niwaombe muwe mabalozi wa kutunza na kuwafichua wanaoharibu vyanzo vya maji.”

Chanzo: Mwananchi