Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Seth aieleza mahakama hajaonana na mke wake kwa miezi sita

14666 Seti+pic TanzaniaWeb

Thu, 30 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mshtakiwa Harbinder Sethi ambaye anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi   ameeleza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa ana miezi sita sasa hajawahi kuonana na mke wake.

Sethi ambaye kwa sasa yupo katika gereza la Ukonga ameyaeleza hayo leo Agosti 30 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Awali Wakili wa serikali, Mwanaamina Kombakono aliieleza mahakama kuwa kesi ya Sethi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi bado haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa.

Baada ya Wakili Kombakono kueleza hayo, Wakili wa Sethi, Dorah Mallaba aliieleza mahakama kuwa bado hawajapata kibali kwa  ajili ya mshtakiwa Sethi kuonana na mkewe.

Wakili Mallaba aliiomba mahakama iruhusu hata kwa dakika tano Sethi aonane na mkewe.

"Naomba mahakama itumie busara kwa kuwa wake wake yupo hapa mahakamani,” amesema Mallaba

Wakili Kombakono baada ya kusikiliza hoja ya wakili Mallaba, aliieleza mahakama kuwa taratibu za kumuona mahabusu zifuatwe.

Hakimu Shahidi amesema taratibu za kuwatunza mahabusu zipo chini ya Magareza na kama kuna jambo lolote mahususi lbasi linatakiwa kuletwa mahakamani.

Hakimu Shahidi ameiahirisha kesi hiyo hadi Septemba 13, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia upelelezi utakuwa umekamilika au la.

Katika kesi hiyo Sethi na James  Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka  12 ya  uhujumu uchumi  ikiwamo kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu , kughushi,  kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na  kutakatisha fedha.

Soma Zaidi:

Wakili alalamika mke wa Seth kuzuiwa kumuona mume wake

Chanzo: mwananchi.co.tz