Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serukamba kamatwa na Takukuru Dodoma

61623 Serukambapic Serukamba kamatwa na Takukuru Dodoma

Thu, 9 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kutokana na tuhuma za kutaka kutoa rushwa kwa wajumbe wa NEC na wapiga kura wake.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Takukuru mkoani Dodoma, Sosthenes Kibwengo, amesema Takukuru inamshikikia mbunge huyo huku ikiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kujiridhisha na makosa hayo.

Kibwengo amesema mtuhumiwa huyo amekutwa maeneo ya Dodoma Hoteli.Amesema mpaka sasa bado yupo mikononi mwa Takukuru jijini Dodoma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live