Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali za mitaa kinara kwa rushwa

RUSHWA Serikali za mitaa kinara kwa rushwa

Thu, 30 Apr 2020 Chanzo: --

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mwanza imesema serikali za mitaa zinaongoza kwa kulalamikiwa dhidi ya vitendo vya rushwa.

Kaimu Mkuu wa Takukuru mkoani Mwanza, Daud Ndyamukama, alisema taasisi hiyo imepokea malalamiko 219 katika kipindi cha Januari hadi Machi, mwaka huu.

"Takwimu zinaonyesha kwa vipindi vitatu mfululizo Januari hadi Machi, serikali za mitaa ndizo zinaongoza kwa kulalamikiwa dhidi ya vitendo vya rushwa,” alisema Ndyamukama.

Kati ya malalamiko hayo, alisema 47 yanahusu serikali za mitaa, wenyeviti, watendaji wa vijiji, mitaa, vitongoji na kata huku idara ya elimu ikiwa na malalamiko 37 na taasisi za fedha 17.

Aidha, alisema malalamiko mengine yanahusu mahakama (16), polisi (16), ardhi (13), vyama vya ushirika (12), afya (12) na 24 kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ununuzi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kilimo, bima, nishati, ujenzi na mifuko ya hifadhi ya jamii.

Pia alisema malalamiko mengine 24 ni kutoka katika taasisi za uhamiaji, ulinzi, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), usafirishaji, asasi za kiraia, ukaguzi, siasa, maliasili, taasisi za dini na sekta binafsi.

Kutokana na malalamiko hayo, Ndyamukama ilitoa wito kwa wananchi kuzingatia makatazo ya vitendo vya rushwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.

Chanzo: --