Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yamsaka muuguzi aliyebaka mgonjwa

83656 Pic+muuguzi Serikali yamsaka muuguzi aliyebaka mgonjwa

Thu, 14 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora.  Wizara ya Afya inafuatilia sakata la muuguzi anayedaiwa

kumbaka msichana mgonjwa na kisha kukimbia kusikojulikana.

Akizungumza na watumishi wa hospitali ya wilaya ya Igunga na viongozi

wa sekta ya afya mkoa wa Tabora, Naibu katibu mkuu (Tamisemi-Afya),

Dk Dorothy Gwajima alisema lengo ni kuona haki inatendeka.

“Pia lazima kurudisha heshima ya sekta hiyo na hospitali ya wilaya ya

Igunga,” amesema.

Ameeleza kuwa anayedaiwa kufanya tukio hilo ni mtu mmoja na hawezi

kuchafua sifa ya sekta nzima ya afya na kutaka hatua zichukuliwe dhidi

ya mhusika.

Akimzungumzia mtumishi mwingine wa hospitali hiyo, anayedaiwa kuomba rushwa ya Sh200,000 na kukamatwa na Takukuru ambapo ana kesi mahakamani,alisema hilo liwe funzo kwa watumishi wa sekta ya afya akisema hospitali sio pango la kuomba rushwa.

Ameonya kuwa watumishi wanapokabiliwa na mkono wa sheria kwa kufikishwa mahakamani inakuwa si mwisho kwani watakumbana na mabaraza yao ya kitaaluma pamoja na kiutawala.

Naye mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli, alisema tayari amemsimamisha kazi muuguzi anayekabiliwa na kesi ya rushwa mahakamani, akisubiri sheria ichukue mkondo wake.

Kuhusu mtumishi anayedaiwa kumbaka msichana mgonjwa alisema kuna hatua zinaendelea na kwamba hawezi kuzisema ni hatua gani kwa sasa.

Naye Katibu tawala mkoa wa Tabora, Msalika Makungu aliwataka watumishi wa sekta ya fya kutambua dhamana waliyo nayo katika kuwahudumia wananchi na kuwataka kuwa mfano mzuri kwa jamii.

Chanzo: mwananchi.co.tz