Upelelezi wa Kesi ya Uhujumu Uchumi namba 27/2021 inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na Wenzake Sita umekamilika ambapo washtakiwa wote watasomewa maelezo ya awali Septemba 16 mwaka huu.
Wakili Mkuu wa serikali Tarsila Gervas ameimbia mahakama ya hakimu mkazi Arusha leo kuwa licha ya upelelezi kukamilika tayari wamepata kibali cha kuridhia mahakama hiyo kusikiliza shauri hilo.
Lengai Ole Sabaya na Wenzake Sita wanakabiliwa na makosa ya uhujumu Uchumi na utakatishaji fedha, makosa ambayo wanadaiwa kuyatenda Januari 22/2021 jijini Arusha ambapo wanadaiwa kujipatia kitita cha shilingi milioni 90 kinyume cha sheria.