Dar es Salaam. Kesi ya uchochezi inayomkabili makamu mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu na wenzake imeshindwa kuendelea kutokana na Serikali kushindwa kuwasilisha jalada mahakamani.
Kutokana na hali hiyo, hakimu Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alionya upande wa mashataka na kuutaka tarehe ijayo ukikishe unakuwa na jalada.
“Tarehe ijayo nataka upande wa mashtaka mje na jalada ili kesi hii iendelee, maana haiwezekani mnasema hamna jalada,” alisema hakimu Simba.
Washtakiwa wengine ni Simon Mkina, Jabir Idrisa na mchapishaji wa kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob kwa wanakabiliwa na mashtaka ya uchochezi.
Kesi hiyo jana ilipangwa kwa ajili ya kusikilizwa maombi yaliyowasilishwa na wadhamini wa Lissu wakiomba mahakama hiyo kutoa hati ya kumkamata, kwa kuwa wao wameshindwa kumpata.
Wadhamini hao, Robert Katula na Ibrahim Ahmed, waliwasilisha maombi hayo Februari 20 wakitaka mahakama hiyo itoe amri ya kumkamata Lissu baada ya jitihada za kumtafuta kushindika.
Pia Soma
- Kauli aliyotoa Bashiru juu ya dola kimantiki ni sahihi
- ACT-Wazalendo ilivyopanga safu yake kuelekea uchaguzi wa 2020
- Meneja wa Diamond athibitisha kukutwa na corona