Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kusimamisha mashahidi 20 kesi ya Sabaya na wenzake

SABAYA3445 660x400 Serikali kusimamisha mashahidi 20 kesi ya Sabaya na wenzake

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumla ya Mashahidi 20 wa upande wa Jamhuri wanatarajiwa kutoa ushahidi katika kesi uhujumu uchumi na utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na Wenzake sita makosa ambayo wanadaiwa kuyatenda Januari 22/2021.

Watuhumiwa hao wamesomewa mashtaka yao baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kuipa mamlaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi.

Katika keshi hiyo namba 27/2021 Lengai Ole Sabaya na Wenzake wanakabiliwa na mashtaka Matano ikiweno ya kuongoza Genge la uhalifu na kujipatia kitita cha milioni 90 kinyume cha sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live