Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kujenga mahabusu ya watoto Mwanza

Mahabusuupiic Data Dr. Dorothy Gwajima

Sat, 30 Jul 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Wanawake na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima amesema wizara yake imetenga kiasi cha Sh400 milioni kwa ajili ya ujenzi wa mahabusu ya watoto wanaokinzana na sheria mkoani Mwanza.

Watoto wanaokinzana na sheria wamekuwa wakitunzwa katika mahabusu tano yaani Tanga, Arusha, Dar es Salaam, Mbeya na Kilimanjaro na kwamba wamekuwa wakirekebishwa tabia huku wakiendelea na masomo.

Waziri Gwajima ameyasema hayo leo Jumamosi, Julai 30, 2022 wakati akifafanua mbele ya waandishi wa habari majukumu ya Wizara na utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

“Kwa kuzingatia mgawanyo wa mahabusu za watoto nchini ambazo ziko mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya na Dar es salaam Serikali imeona umuhimu wakujenga mahabusu ya watoto mpya katika Mkoa wa Mwanza ili iweze kuhudumia mikoa ya kanda wa ziwa ambapo milioni 400 zimetengwa kutekeleza ujenzi huo,” amesema Dk Gwajima.

Akifafanua zaidi kuhusu mahabusu za watoto wanaokinzana na sheria, amesema Wizara inasimamia mahabusu zenye idadi ya watoto 47 ili kuwatenga watoto wote wanaokinzana na sheria na mahabusu za watu wazima.

Amesema majengo ya mahabusu za watoto yanahitaji ukarabati hivyo, serikali imetenga Sh300 milioni kukarabati mahabusu za watoto katika Mikoa ya Mbeya na Arusha.

Waziri Gwajima amesema Serikali itaendelea kutoa huduma ya marekebisho ya tabia kwa watoto wote waliokinzana na Sheria na hatimae kupatikana na hatia kwa makosa waliyoyatenda.

“Watoto hawa ambao hawapelekwi magereza baada ya kuhukumiwa, Serikali huwatunza katika shule ya mabadilisho iliyoko Irambo Mbeya ambapo kwa sasa kuna watoto 36 wanaorekebishwa tabia. Serikali imetenga kiasi cha Sh615.68 milioni kwa ajili ya huduma ya chakula, mavazi, malazi, afya, elimu na huduma zote za msingi kwa mtoto,” amesema Dk Gwajima.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz