Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuanza kutoa ushahidi kesi ya Wakili Madeleka Juni 21

Madeleka Pic Data Serikali kuanza kutoa ushahidi kesi ya Wakili Madeleka Juni 21

Thu, 19 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya kuchapisha habari za uongo kinyume na kifungu cha 16 cha sheria ya mtandao ya mwaka 2015 inayomkabili Wakili wa kujitegemea, Peter Madeleka, imeshindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu ya Mkazi Kisutu.

Kesi hiyo ya jinai namba namba 69/ 2022 imeshindwa kuendelea Mei 18, 2022, baada ya Hakimu Mkazi anayesikikiza shauri hilo, Rhoda Ngimilanga kupata dharura.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ester Martin akishirikiana na Mwanaamina Kombakono na Caroline Materu, amedai kuwa shauri hilo liliitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka,  lakini hakimu anayesikiliza kesi hiyo amepata dharura na hivyo wanaomba terehe nyingine.

"Upande wa mashtaka tayari tunao mashahidi watatu hapa mahakamani, lakini hakimu anayesikiliza kesi hii amepata dharura, hivyo tunaomba kuahirisha kesi hii hadi terehe nyingine kwa ajili ya kuendelea" amedai Wakili Martin.

Kwa upande wake wakili wa utetezi Paul Kisabo, yeye ameiomba Mahakama hiyo kutoa ahirisho la mwezi mzima kwa sababu wiki ijayo Chama Cha Mawakili wa Tanganyika( TLS) kitakuwa na uchanguzi Mei 27, 2022 hivyo huwa kuna kuwa maandalizi ambayo yataanza Mei 23, 2022.

Hakimu Tarimo baada ya kusikiliza maelezo hayo, ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 21, 2022, itakapoendelea na mshtakiwa yupo nje kwa dhamana.

Advertisement Kwa mara ya kwanza, Madeleka amefikishwa mahakamani hapo Mei 5, 2022 kujibu shtaka linalomkabili.

Katika kesi ya msingi, Madeleka ambaye ni mkazi wa AICC Kijenge, mkoani Arusha anadaiwa kutenda kosa hilo, April 18, 2022 katika maeneo yasiyojulikana katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Siku hiyo ya tukio, mshtakiwa kupitia akaunti yake ya mtandao wa Kijamii ya Twitter yenye jina la PMadeleka alichapisha habari lililosema " Huyu ndiye ERENEUS MWESIGWA Ofisa Uhamiaji anayeratibu njama za kuniua kwenye GROUP LA WHATSAPP pamoja na Maofisa Uhamiaji wenzake", huku akijua kuwa taarifa hizo ni za uongo.

Mshtakiwa baada ya kusomewa shtaka linalomkabili, amekana kutenda kosa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live