Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali bado inajadiliana na bosi wa JATU

Jatu Picbnn Serikali bado inajadiliana na bosi wa JATU

Mon, 19 Jun 2023 Chanzo: mwanachidigital

Serikali imesema bado inaendelea na majadiliano ya kuimaliza kesi dhidi ya Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya (33) anayekabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kujipatia Sh5.1 bilioni kwa njia ya udanganyifu.

April 24, 2023 Gasaya kupitia wakili wake, Nafikile Mwamboma, aliieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu kuwa amemwandika barua ya kukiri na kuomba apunguziwe adhabu, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP).

Kutokana na hali hiyo, Mahakama hiyo ilitoa siku 30 kwa upande wa mashtaka kuanza majadiliano ya kuimaliza kesi hiyo kwa njia ya majadiliano na DPP.

Leo Jumatatu Juni 19, 2023, Wakili wa Serikali Frank Michael ameieleza Mahakama hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate kuwa Serikali bado wanaendelea na mchakato wa majadiliano dhidi ya Gusaya kwa lengo la kuimaliza kesi, hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Kabate baada ya kusikiliza maeneo hayo, ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 3, 2023 itakapoitwa kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama upande wa mashtaka wameshakamilisha majadiliano.

Katika kesi ya msingi, mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kujipatia Sh5.1 bilioni na kutakatisha kiasi hicho katika kesi ya uhujumu uchumi namba 8/2023.

Chanzo: mwanachidigital