Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sendeka akataa kukubali maelezo ya mama anayedai kumla mtoto

85600 Pic+benk Sendeka akataa kukubali maelezo ya mama anayedai kumla mtoto

Sun, 24 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Jeshi la Polisi Kanda ya Dara es Salaam linamshikilia Halima Juma (23) mkazi wa Chalize kwa tuhuma za wizi katika akaunti za wateja wa benki kutoka katika machine za kutolea fedha (ATM).

Kamanda wa Kanda, Lazaro Mambosasa alisema Novemba 11 akiwa katika mashine ya ATM ya tawi la benki ya CRDB Mbagala, polisi aliyekuwa zamu alimtilia shaka binti huyo.

Alisema binti huyo alijifanya akiwasaidia wazee na wastaafu ndani ya chumba cha mashine hiyo, lakini lengo lake lilikuwa kuchukua namba za siri za wazee hao na kuwabadilishia kadi.

“Huyu mwanamke anajifanya anawasaidia wazee. Anaandaa kadi feki na kuiweka pembeni, huchukua namba ya siri kuwabadilishia kisha yeye kubaki na kadi halisi,” alisema Mambosasa.

Alisema baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa alipekuliwa na kukutwa na kadi 23 za wateja wa benki tofauti zikiwa katika pochi yake.

“Alikutwa na kadi saba za CRDB, sita za NMB, mbili za NBC, mbili za benki ya posta, moja ya ACB, moja ya Stanbinc, moja ya DTB na nyingine moja ya benki ya Equity,” alisema.

Kamanda Mambosasa ametoa tahadhari kwa wazee na wastaafu wanaoenda kutoa fedha katika mashine hizo kuwa makini na watu wasiowafahamu wanaotaka kuwasaidia kutoka fedha.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limetoa tahadhari kwa wakazi wa jiji kuwa makini na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ili kuepuka majanga yanayoweza kuepukika.

“Wananchi wote wanatakiwa kuwa makini na watoto wadogo wanaohitaji uangalizi wa karibu, kujiepusha kupita kwenye madimbwi ya maji na mito midogomidogo ili kuepusha madhara,” alisema.

Amesema hadi sasa jeshi hilo limepokea taarifa za vifo vya watu wawili na mmoja kujeruhiwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Dar es Salaam.

Chanzo: mwananchi.co.tz